emblem

Tanzania Standard Newspapers

Serikali yaahidi kukamilisha mradi wa TSN


Serikali yaahidi kukamilisha mradi wa TSN


DODOMA - Serikali imeahidi kushirikiana na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ili kuhakikisha mradi wa kiwanda cha uchapaji kisasa unakamilika kwa wakati. Hatua hiyo inalenga kuongeza ufanisi wa kampuni hiyo na kuimarisha ushindani wake sokoni.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Paramagamba Kabudi, jijini Dodoma, alipohutubia wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo katika semina maalum iliyoandaliwa kwa ushirikiano na TSN na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Waziri Kabudi amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari vya umma katika kuchochea maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Husna Sekiboko, amesema kikao hicho kiliandaliwa ili kujifunza mikakati ya maendeleo ya taasisi hizo na kujadili mbinu bora za kuboresha huduma kwa jamii.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TSN, Asha Dachi amesema kampuni hiyo imeanza kuchukua hatua mbalimbali ya kuhakikisha kuwa inateka soko la habari mtandao ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea duniani kote kwa kuwekeza nguvu kubwa zaidi katika uzalishaji wa gazeti mtandao.