KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) imetoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa Wanawake wa Gereza la Mahabusu Segerea, Dar es salaam.
Msaada huo umetolewa na Watumishi wanawake wa TSN ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Wanawake hao walitembelea gereza hilo leo na kutoa msaada wa magodoro, sukari, taulo za kike(pads) na taulo za watoto(diapers) na nguo mbalimbali.