emblem

Tanzania Standard Newspapers

Uteuzi wa Wajumbe wa Bodi TSN


Uteuzi wa Wajumbe wa Bodi TSN


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi ameteua wajumbe sita wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN). Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika wizara hiyo imeeleza kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na uteuzi wao umeanza tangu Julai 22, mwaka huu Wajumbe wa bodi hiyo ni mkufunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dk Chisulingwe Khadudu, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda na mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk Ayub Rioba. Wengine ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani wa kilichokuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Elimbora Muro, aliyekuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Masoko Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Deogratius Kwiyukwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zamaradi Kawawa.