emblem

Tanzania Standard Newspapers

PSSSF na TSN Kuimarisha Ushirikiano wa kimkakati katika Utendaji.

  • May 21, 2026

PSSSF na TSN  Kuimarisha Ushirikiano wa kimkakati katika Utendaji.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeahidi kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN),katika utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa lengo la kufikia wateja wake.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Makao makuu ya TSN Bi  Maria Lupondo Meneja wa PSSSF Kanda ya Temeke, amesema kuwa amefurahishwa na taarifa aliyoipata kutoka kwa Menejiment ya TSN kutokana  na ufafanuzi wa  majukumu yanayotekelezwa na TSN.

“Sikuwahi kujua kuwa TSN mnatekeleza majukumu makubwa kiasi hiki, sisi tunajua kuwa TSN ni wachapaji wa Magazeti tu ,kumbe bado mnashughuli nyingi mnafanya nje ya uchapaji wa magazeti. PSSSF kuna kazi nyingi za kufanya na TSN sasa naomba tufanye kazi kimkakati hasa katika uchapaji wa nyaraka mbalimbali ambazo ni nyenzo za uelemishaji”

Naye Bi Colleta Mnayamani ambaye ndio alikuwa mkuu wa msafara amesema PSSSF ipo tayari kutumia majukwaa ya kidigitali ya TSN Pamoja na kupata ushauri wa kitaalam katika kuhabarisha umma kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na PSSSF.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Habari wa TSN, Bw.  Majaliwa Christopher, aliwaeleza ni kwa namna gani TSN inaweza kutumia majukwaa yake kufikisha taarifa sahihi kwa umma na kwa wakati hasa elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo wa hifadhi ya jamii nchini.

Aidha alifafanua umahiri na uzoezifu wa TSN katika masuala ya habari huku akiwahakikishia maafisa hao ufanisi katika utekelezaji wa makubaliano ambayo yatatekelezwa kwa wakati na kwa kiwango watakavyokuwa wamekubaliana katika mkataba kwani matokeo ya kazi yataleta tija kwa pande zote mbili.

“ TSN Pamoja na majukumu mengine lakini suala la kusukuma ajenda za serikali ili zifikie jamii kwa mapana yake ni jukumu letu,hivyo tuendelee kushirikiana na tupotayari kwa utekelezaji naamini ziara hii ya leo italeta manufaa makubwa, kwani imeongeza hari kwa TSN kwakuwa kuja kwenu hapa kumeongeza kujuana zaidi. ”

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Biashara TSN, Bi. Soter Salema, alielezea maeneo ya kimkakati yatakayokuwa fursa muhimu kwa ushirikiano wa kikazi. Miongoni mwa maeneo hayo ni uzinduzi wa gazeti mkononi litakalo fahamika kama (TANePres), majukwaa ya kutoa elimu kwa umma, huduma za maktaba, majukwaa ya kidijitali, huduma za uchapaji pamoja na huduma za ushauri wa kitaalamu katika masuala ya uandishi wa habari.

Kikoa hicho kimetokana na ziara iliyofanywa na Maafisa uhusiano waliotembelea TSN kwa lengo la kuongeza mahusiano Pamoja na kujifunza namna TSN inavyotekeleza majukumu yake.